Quantcast
Channel: Global Voices in Swahili » Teknolojia
Viewing all 55 articles
Browse latest View live

Mazungumzo ya GV: Namna ya Kutengeneza Video za Utetezi na Mabadiliko

$
0
0

Je, unatumia video kuifanya kampeni kuwa uhalisia? Je, una mpango wa kusimulia habari zako au kutengeneza filamu za shughuli fulani kwa kutumia kamera -au simu yako?

Kwenye toleo hili la Mazungumzo ya #GV , Matisse Bustos Hawked na Bukeni Waruzi kutoka shirika la Witness na Laura Morris kutoka Rising Voices kujadili masuala muhimu ya kuzingatia wakati wa kutengeneza video kwa ajili ya utetezi, na namna ya kukabiliana na matatizo ya mara kwa mara yanayojitokeza kwenye uandishi wa habari za kiraia, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwenye maeneo yenye mtandao usio na kasi na namna ya kuifikia hadhira kwa njia za kitekilojia (za juu na zile za kawaida).

Pia walijadili umuhimu wa kuhakiki maudhuri na mbinu bora za kufanya kazi hiyo na pia kujibu maswali yenu kupitia kipindi cha maswali na majibu.


Jiunge na IGF Japan Kujadili Utawala wa Mtandao

$
0
0

IGF Japan, hatua ya maendeleo nchini Japani ya Jukwaa la Utawala Mtandao, ambapo watu wanaojihusisha mtandaoni huja pamoja kujadili changamoto za utawala wa mtandao, ulifanyika Machi 14, 2014 katika chuo kikuu cha Aoyama Gakuin. Vikao vitajadili mada kama vile data binafsi na faragha, kujitokeza kwa tovuti za hali ya juu nchini Japan, na mwenendo wa mtandao wa kimataifa.

Mazungumzo ya GV: “Mtandao wa Twita” wa Siri wa Kimarekani Nchini Cuba

$
0
0

Mpango wa siri wa Marekani wa kubadili utawala nchini Cuba wenye huduma ya ujumbe inayofanana na Twita iitwayo ZunZuneo sasa unaangaliwa kwa mashaka baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa maelfu ya wa-Cuba walidanganyika kujisajili kupata huduma hizo.

Je, kutakuwa na madhara kwa wanaharakati wa kidijitali duniani kote? Wengine wana mashaka gatua hiyo inaweza kusababisha hali ya kutokuaminiana na kufuatiliwa kwa mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii katika nchi zao.

Majadiliano ya kina na: Sana Saleem, Ivan Sigal na Solana Larsen.

Uchaguzi Mkuu wa India 2014: Kampeni Kwenye Mitandao ya Kijamii

$
0
0

Mitandao ya kijamii imekuwa ni sehemu ya ugunduzi na ubunifu. Milind Deora [Waziri wa Muungano na Mbunge wa Mumbai Kusini] anatamba kuwa mgombea wa kwanza kupatikana kwa wapiga kura wake kwenye mtandao wa WhatsApp na BBM, na huko anajadili mpango kazi wake ikiwa ni pamoja na shughuli zake na mipango yake. Kama ilivyo kwa Poonam Mahajan, Deora vile vile ana ukurasa wa Facebook na Twita zikiwa zimeunganishwa kutoa taarifa zake.

Social Samosa anapitia kwa kina namna wanasiasa wa Kihindi mjini Mumbai waliamua kuingia kwenye mitandao ya kijamii kufanya kampeni zao.

Shirika la Friedrich Ebert Lachapisha Ripoti ya Matumizi ya Mitandao ya Kijamii Nchini Cameroon

$
0
0

Shirika la Friedrich Ebert limechapisha ripoti ya utafiti kwenye matumizi ya mitandao ya kijamii nchini Cameroon:

Kwa kiwango kipi, kwa malengo yapi na kwa akina nani basi mitandao ya kijamii kama Twita, Facebook, Blogu, Linkedin, nk. inatumika nchini humo? Kujua majibu ya maswali hayo, Shirika la Friedrich Ebert limetoa taarifa ya matumuzi ya mitandao ya kijamii nchini Cameroon…

Kwa upande wa umaarufu wa mitandao ya kijamii, kama ilivyo kwingineko, Facebook ndiyo zana maarufu zaidi nchini Cameroon. Baadhi ya makundi ya Ki-Camerron yana hadi wafuasi 20.000 na zaidi. Na kwa hali ya kushangaza ni umaarufu wa mtandao wa Linkedin. Karibu watumiaji wanne kati ya watano wa mtandao wa intaneti nchini Cameroon wamejiunga na huduma hiyo, ikilinganishwa na asilimia tatu tu kwenye nchi jirani ya Naijeria. Utafutaji wa kazi na fursa za ajira inaweza kuwa sehemu ya majibu ya hali hii. Mtandao mwingine unaopata umaarufu nchini humo ni Twita. Cameroon kwa sasa ni kati ya nchi kumi maarufu za kiafrika zenye ujazo mkubwa wa twiti, ingawa twiti nyingi zinatokea kwenye miji ya Douala na Yaoundé. Kwa kulinganisha, bado kuna uchanga wa kublogu, kwa kuangalia mahitaji makubwa ya muda na maudhui. Hata hivyo, ingawa wanablogu wa Cameroon ni wachache kwa idadi, wana uwezo mkubwa kimaudhui na viwango. Baadhi ya blogu maarufu zaidi barani Afrika zinatoka Cameroon, baadhi zikiwa zinaratibiwa na na muungano wa wanablogu uitwao “Collectif des Blogueurs Camerounais.” Kwa nyongeza, tayari jitihada za kiubunifu zimefanyika na haina shaka kuwa jitahada hizo zitaongeza kuenea kwa mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi ambayo kwa sasa inasaidia kukuza shughuli za kiuchumi.

Mradi Wa Kutumia Simu za Mkononi Kuhamasisha Usomaji

$
0
0

Lauri anaandika kuhusu mradi uliopo Afrika Kusini, Mfuko wa Usomaji wa FunDza, unaotumia teknolojia ya simu za mkononi kuhamasisha tabia ya kusoma kwa watoto:

Kinachofurahisha, hata hivyo, ni pale Waafrika wanapopata majibu ya kiubinifu kwa matatizo yao. Mradi wa FunDza ni mfano moja wapo. Simu za mkononi zimeenea sana nchini Afrika Kusini na FunDza wanalenga kuwasaidia watoto wapende kusoma. Ninajisikia fahari kuandika mara kwa mara kwa ajili yao.

Namna inavyofanya kazi ni kwamba hadithi inaanza Ijumaa. Kila hadithi ina sura saba na sura moja inatumwa kwenda kwennda kwenye simu za watoto kila siku. Hapa ni ukurasa wa mwandishi wenye hadithi zote nilizoandika kwenye mradi wa FUnDza. Bofy kwenye hadithi yangu kuona maoni yanayoanhwa na wasomaji. Watoto wanasoma na kuhusika na hadithi! Ninadhani hatua hii ni kubwa!

Mazungumzo ya GV: Moja kwa Moja kutoka Kombe la Dunia la Mtandaoni

$
0
0

Mazungumzo ya GV juma hili yanakujia moja kwa moja kutoka São Paulo, Brazil mahali ambapo wawakilishi wa serikali, vyama vya kiraia na mashirika wamekusanyika kutoka duniani kote wiki hii katika kituo cha mkutano cha NETMundial ili kutengeneza ‘mwongozo’ wa utawala wa kidunia wa mtandao wa intaneti katika kipindi hiki cha baada ya sakata la [Edward] Snowden.

Ellery Biddle wa Global Voices Utetezi anaungana na Marianne Diaz na Ben Wagner.

Rwanda: Mema, Mabaya na Matumaini

$
0
0
-Paul Kagame, President of Rwanda  at the World Economic Forum on Africa 2009 in Cape Town, South Africa- via wikipedia cc-license-2.0

Paul Kagame, Rais wa Rwanda, akiwa kwenye Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Afrika uliofanyika mwaka 2009 jijini Cape Town, Afrika Kusini- kupitia wikipedia cc-license-2.0

Rwanda bado inauguza makovu ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyoteketeza maisha ya watu kati ya 800,000 na milioni moja, ikiwa ni asilimia 80 ya idadi ya watu wa kabila la Watutsi ikiwa ni pamoja na Wahutu wengi. Inakadiriwa kuwa sehemu moja ya sita ya idadi ya raia wa nchi hiyo waliuawa ndani ya majuma kadhaa.

Miaka ishirini baadae mchakato wa maridhiano bado una safari ndefu kufikia mafanikio. Rais Paul Kagame anatuhumiwa kuwadhibiti wapinzani wake, moja yapo ya vitendo vingi vya uvunjifu wa haki za binadamu. Lakini jitihada za kujenga upya nchi hiyo zimeanza kuleta matokeo yanayoonekana.

Habari Njema

Moja ya mafanikio makubwa ya nchi ya Rwanda ni kukua kwa usawa wa kijinsia katika maeneo mengi. Idadi ya wanawake kwenye bunge la Rwanda, ni asilimia 64, ambayo ni idadi kubwa kuliko kwenye mabunge mengine duniani, kwa mujibu wa orodha ya 2014 ya Umoja wa Mabunge katika nchi 189.

Louis Michel, waziri wa zamani nchini Ubeligiji na kamishina wa Umoja wa Ulaya, alibainisha kwenye blogu yake [fr]:

Ces résultats sont spectaculaires : en moins de dix ans plus d’un million de personnes ont été sorties de la pauvreté extrême et le pays a enregistré un taux de croissance économique stable de 8% par an. Plus de 95% des enfants ont aujourd’hui accès à un cycle complet d’éducation primaire, la mortalité infantile a été réduite de 61% tandis que les trois quart de la population ont accès à l’eau potable. Enfin, près de 50% des femmes ont accès à un moyen de contraception, ….. Cela fait du Rwanda l’un des très rares pays d’Afrique qui pourra affirmer avoir atteint la quasi-totalité des OMD en 2015. 

Matokeo haya ni ya ajabu: kwa muda usiofika miaka kumi, zaidi ya watu milioni moja wameinuliwa na kuuaga umasikini uliokidhiri na nchi inaonekana kuwa na uchumi imara na unaokua kwa asilimia 8 kwa mwaka. Leo zaidi ya asilimia 95 ya watoto wanapata elimu ya msingi bora, vifo vya watoto vimepungua kwa asilimia 61, na robo tatu ya raia wa nchi hiyo wanapata maji safi. Mwishoni, takribani asilimia 50 ya wanawake wanapata huduma za uzazi wa mpango…hii ikiwa na maana kuwa Rwanda ni moja ya nchi chache za Afrika ambazo zinakaribia sana kufikia Malengo ya Milenia mwaka 2015.

Mpango wa kwanza wa maendeleo wa miaka mitano kwenye eneo la teknolojia mpya [fr], ulibuniwa mwaka 2001, umeonyesha mafanikio makubwa. Wakati wa awamu ya pili ya mpango huo, iliyoishia mwaka 2010, Rwanda ilishuhudia asilimia 8,900 ya ongozeko la watumiaji, ukifananisha na asilimia 2,450 kwenye sehemu nyingine barani Afrika na asilimia 44 duniani. Jarida la African Renewal, linalomilikiwa na Umoja wa Mataifa, liliandika kwamba maeneo manne ya sekta ya umma (mawaziri, mawakala, majimbo na wilaya) na takribani theluthi ya sekta binafsi imeunganishwa na mtandao wa intaneti. Mji mkuu wa Rwanda, Kigali unafanya vyema kwenye maendeleo ya mfumo wa rada na mawasiliano ya anga kwenye eneo lote.

Rais Kagame anashikilia msimamo kwamba “intaneti ni huduma inayohitajika kwa umma kama ilivyo kwenye maji na umeme.” Kwa ushirkiano na kampuni ya mawasiliano ya Rwandan Telecentre Network (RTN), serikali imetekeleza mpango wa maendeleo ya upatikanaji wa huduma ya intaneti katika maeneo ya vijijini. Taarifa [fr] iliyochapishwa kwenye mtandao wa balancingact-africa.com inasema:

Rwandan Telecentre Network (RTN) s’est rallié aux efforts du gouvernement et s’est engagé à créer un réseau national de 1 000 centres TIC d’ici la fin de 2015 et à former du personnel local. 

Kampuni ya Rwandan Telecentre Network (RTN) ikishirikiana na jitihada za serikali, imekusudia kujenga mtandao wa kitaifa wa vituo 1,000 vya teknolojia mpanga ifikapo mwaka 2015 na kuendesha mafunzo ya wataalam wa ndani.

Dalili za maendeleo ya kiteknolojia ni kwamba Rwanda ni nchi yenye mafanikio ya juu zaidi miongoni mwa nchi za Afrika zinazoshiriki kwenye mpango uitwao Kompyuta Moja kwa Kila Mtoto. Kwa mujibu wa ukurasa wa OLPC   :

 Kufikia mwisho wa mwaka 2012, kompyuta 210,000 zimesambazwa kwenye shule 217 nchini kote. Mwaka 2013: Kompyuta 210,000 = 110,000 (kabla ya 2012) +100,000 (2012)[zilisambazwa] nchini 

Habari za Matumaini

Baada ya mauaji ya kimbari, nchi hiyo ilichukua hatua za kisheria, kujenga Tume ya Kitaifa ya Umoja na Maridhiano (NURC). Tume hiyo, iliyoanzishwa mwaka 1999, inakusudia kuchangia kwenye hatua za utawala bora; kukuza mshikamano, maridhiano na ushirikiano wa kijamii miongoni mwa Wanyarwanda; na kujenga nchi ambayo kila mmoja ana haki sawa.

Susan Thomson, profesa wa stadi za siasa za Afrika kwenye chuo cha Hampshire nchini Marekani, aliandika kwenye makala haya [fr] yaliyochapishwa kwenye mtandao wa machapisho ya kitaaluma wa Cairn.info:

Sous la férule du RPF, l’État postgénocide a largement contribué à restaurer la paix, l’unité et la réconciliation aux quatre coins du pays. L’appareil d’État rwandais, solide et centralisé, a facilité une reconstruction rapide. À la différence de La plupart des autres États africains, le Rwanda est capable d’exercer son contrôle territorial avec une efficacité extrême. Les institutions de l’État ont été restaurées. 

Chini ya utawala wa [chama tawala] cha Patriotic Front, nchi hiyo iliyowahi kukumbwa na mauaji ya kimbari imepiga hatua kubwa katika kurejesha amani, umoja na maridhiano nchini kote. Muundo wa serikali ya Rwanda, ulio imara na unganishi, umewezesha mabadiliko ya haraka. Tofauti na nchi nyingi za Afrika, Rwanda inaweza kutumia mamlaka yake ya ndani kwa mafanikio makubwa. Taasisi za kiserikali zimekarabatiwa.

Taasisi ya Amani ya Rwanda (RPA) ni mfano wa maendeleo hayo, Taasisi hiyo mwaka 2009 kwa kutumia misaada ya kifedha kutoka Japan na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, imekuwa na mpango wa kufanya tafiti na kujenga na kutekeleza mafunzo ya kitaalam na mipango ya kielimu inayotambulika kimataifa. Lengo ni kuwajengea ujuzi unaotakiwa watumishi wa jeshi, polisi na watumishi wengine wa umma ili kukabiliana na changamoto zilizopo na masuala ya amani na usalama kwa siku za usoni barani Afrika.

Habari Mbaya

Kwa bahati mbaya, kazi hii inayoleta matumaini imefukiwa kwenye kaburi la ukiukwaji wa haki za binadamu unaoripotiwa na makundi ya utetezi. Vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu zimekuwa vikitokea kwa miaka mingi. Mwaka 2012, baada ya kutuma wajumbe kadhaa kwenye nchi hiyo, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International liliishutumu nchi hiyo kwa vitendo hivyo:

Kati ya mwezi Machi 2010 na Juni 2012, Amnesty International ilikuwa na matukio 45 ya kukamatwa kwa wtau kinyume cha sheria na shutuma 18 ya utesaji au vitendo visivyo vya kiungwana kwenye Camp Kami, kambi ya kijeshi ya Mukamira, na kwenye nyumba salama kwenye jiji la Kigali. Wanaume walikamatwa na J2 katika kipindi cha kati ya siku 10 na miezi kadhaa bila kuonana na wanasheria, madaktari na wanafamilia.

Matukio ya kuuawa kisiasa kwa wapinzani [fr] yamekuwa yakiripotiwa nje ya nchi hiyo. Waandishi wa habari na viongozi wa zamani wa kisiasa walio karibu na rais wa Rwanda wamekuwa wakikamatwa na kuuawa [fr]. Matukio ya ukamataji ya hivi karibuni yalithibitishwa mwanzoni mwa mwezi Aprili 2014.

Singer and activist Kizito Mihigo - Public Domain

Mwimbaji na mwanaharakati Kizito Mihigo – Picha kwa matumizi ya umma

Tovuti ya arretsurimages.net [fr] iliripoti kukamatwa kwa mwimbaji maarufu Kizito Mihigo, mhangan wa mauaji ya kimbari, na watu wengine watatu, akiwemo mwanandishi wa habari kwa tuhuma za kupanga shambulizi la bomu kwenye jengo moja jijini Kigali. Kizito Mihigo, hata hivyo, anafahamika kwa uanaharakati wake kwa masuala ya amani. Alianzisha Asasi isiyo ya Kiserikali kwa ajili ya kutoa elimu ya amani. Blogu yake [fr] imeeandika:

Depuis l'année 2003, il a œuvré pour le pardon, la réconciliation et l'unité dans la diaspora rwandaise en Europe. En 2010 quand il est rentré au Rwanda, il a Fondé la Fondation KMP (Kizito Mihigo pour la Paix), une ONG rwandaise qui utilise l'art (musique, theatre poesie, ..) dans l'éducation à la Paix, à la Réconciliation et à la Non-violence après le génocide. 

Tangu mwaka 2003, amekuwa akifanya kazi za kuhamasisha watu kusameheana, kuridhiana na kuungana hususana kwa raia wa nchi hiyo waishio ughaibuni barani Ulaya. Aliporejea Rwanda mwaka 2010, alianzisha Mfuko wa Amani wa Kizito Mihigo, AZISE inayotumia sanaa (muziki, maonyesho, ushairi…) kuelimisha kuhusu amani, maridhiano na kuepuka matumizi ya nguvu baada ya mauaji ya kimbari.

Mwimbaji huyo alipatwa na hatia, lakini mashaka makubwa  [fr] yanazunguka maeneo mengi ya kesi hiyo.

Zaidi, kwa miaka kadhaa iliyopita Kigali imekuwa mahusiano duni ya kidiplomasia [fr] na nchi nyingine kadhaa. Nchi ambayo iliwahi kuwa kipenzi cha nchi za Magharibi, Rwanda sasa imeanza kuwa eneo la kukwepwa na inakosa misaada ya kijeshi [fr] pamoja na ile ya kimaendeleo. Mahusiano ya kidiplomasia na Afrika Kusini yamekuwa mabaya kufuatia mauaji ya kisiasa ya wapinzani waliokuwa nchini humo. Tayari kumekuwa na matukio ya kuwafukuza wanadiplomasia  [fr] katika pande hizo mbili.


Taarifa ya Maendeleo ya Kiteknolojia Barani Afrika

$
0
0

Erik anatushirikisha taarifa 5 kuhusu mwenendo wa teknolojia barani Afrika:

Nimeendelea kutamani kuandika makala za blogu kuhusu taarifa hizi moja baada ya nyingine, nyingi zikihusu Afrika, lakini inaonekana sitaweza. Badala yake, nitaweka kiungo cha kila moja wapo, inayoonekana, na maneno machache ya kwa nini ni muhimu kuzisoma.
1. Taarifa ya Akamai kuhusu “Hali ya Mtandnao wa Intaneti” ya mwaka 2013.

[Pakua [download] Taarifa ya Akamai, PDF]

Ina taarifa nzuri kuhusiana matumizi ya intaneti duniani, pamoja na mwenendo wake. Katika bara la Afrika, hata kama kuna maendeleo zaidi nchini Kenya, wote tunaona maendeleo pia yanayoonekana katika nchi za Afrika Kusini, Misri na Moroko. Hata hivyo, kuna mchoro wa Ericsson kuhusu matumizi ya mtandao wa si-waya.

Tovuti 50 Zilizotembelewa Zaidi Nchini Kenya

$
0
0

Je, unajua ni tovuti gani maarufu zinazotembelewa zaidi nchini Kenya? Soka posti ya James Wamathai kwenye blogu yake kufahamu zaidi:

Mengi yamebadilika tangu mwezi Januari, wakati nilipotoa orodha ya tovuti maarufu zaidi nchini Kenya. Tovti ya Budget airline Jambo Jet ilizinduliwa, gazeti linalomilikiwa na kampuni ya NMG liitwalo Nairobi News lilizinduliwa na kufanikiwa, tovuti ya burudani ya izvipi nayo ilianzishwa na Sauti Sol ilitoa video ya wimbo wao mpya iliyoibua mjadala mkali, lakini ilijipatia umaarufu, ‘Nishike”.

Kwenye orodha ya tovuti maarufu, kuna mabadiliko kadhaa kama unavyoona hapa.

Kenyan Post imeipiku Ghafla kama blogu maarufu zaidi nchini Kenya
Jumia, KRA, Career Point Kenya, Helb na Techweez zimepanda chati.
Niaje, The Star, Orange na Michezo Afrika zimeshuka umaarufu.
Ben Kiruthi, KU, Kenya Today na Kopo Kopo zimeingia kwenye orodha ya 50 bora.

Kijana Huyu Mwenye Asili ya Zambia Awa Mwanafunzi wa Kwanza Kuwa Mtalaam wa Kutegemewa na Microsoft

$
0
0

Kijana mwenye asili ya Zambia, lakini anayeishi Uingereza mwenye miaka 15 Samkeliso Kimbinyi anatengeneza zana za kupiga soga mtandaoni kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano na hivyo kuwa mmoja wa wataalam wadogo zaidi waliobobea na wanaotumiwa na kampuni ya Microsoft barani Ulaya.

Kijana huyo mdogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Sam, mwanafunzi wa darasa la 10 (sawa na sekondari ya juu) kwenye Chuo cha Teknolojia (UTC) huko Reading, mji ulioko nje kidogo ya London. Kwa sasa ni Mtaalam Anayekubalika na Microsoft na ana vyeti vya Ufundi vya Microsoft (MTA) katika maeneo saba ikiwa ni pamoja na Mafunzo ya Msingi za Zana, Mafunzo ya Uundaji wa Program za Windows na yale ya utengenezaji wa mifumo (OS).  

Kimbinyi pia ameunda zana tumizi (app) iitwayo Lite kwa simu zenye zana ya Windows na mpaka sasa ameendelea kupata maoni chanya kwa kazi hiyo.

Sam Kimbinyi's Twitter profile photo.

Picha ya Sam Kimbinyi imechukuliwa kwenye wasifu wake wa Twita.

Global Voices Online ilikutana naye kupitia barua pepe na kutaka kujua kutoka kwake moja kwa moja kuhusu mafanikio yake:

Mwezi Machi mwaka huu, nilikuwa na fursa ya kukutana na wafanyakazi wa Ofisi ya Microsoft pale Seattle, ambao walikuwa Uingereza kwa siku moja kama sehemu ya ziara yao ya Ulaya wakizungumza na wateja wao wanaopata mafunzo kwenye Chuo chao cha Taknolojia na Mawasiliano cha Microsoft. Walikuwa ni wale wa timu ya Mafunzo -Mkurugenzi Mwandamizi Tim Sneath, Mkurugenzi wa Program za Mafunzo Keith Loeber na Mkurugenzi wa Maudhui Briana Roberts.

Mnamo Mwezi Mei 26th 2014 nilichapisha toleo la kwanza la zana ya App—Lite—on ya simu zenye mfumo wa Windows. Nilipata wazo la kutengeneza zana tumizi hii baada ya kutumia masaa mengi nikitafuta zana ambayo ingenisaidia kufanya kazi zangu bila kujaa matangazo mengi. Hatimaye, baada ya kushindwa kupata nilichotaka, niliamua kutengeneza yangu mwenyewe. Siku nane baadae na baada ya kukosolewa sana na Jumuiya ya Reddit ya Simu za mfumo wa Wondows, nilipata habari njema za mipakuo [downloads] ipatayo 300 na wengine waliipa alama za juu kwamba inafaa. Baada ya muda, ikawa kwenye kundi la “Mpya na Inapata Umaarufu” kwenye sehemu ya mauzo ya bidhaa mtandaoni.

Mbeleni ninatarajia kutoa zana tumizi zaidi na kuendelea kujifunza zaidi fani ya Sayansi ya Kompyuta chuoni.

Kwenye kijarida cha chuoni kwake, Kimbinyi alinukuliwa alisema:

Mafunzo Microsoft yanajaribu kutumia kile tunachokisoma darasani, lakini yamenipa uelewa mpana wa ujenzi wa programu na namna tasnia hiyo ilivyo pana. Ufahamu wangu mpya ulikuwa wa muhimu sana tulipotengeneza zana tumizi wakati wa mradi wa mwajiri wa Microsoft; tukaishia kuunda zana [app] bora zaidi.

Microsoft ilimpongeza Kimbinyi kwenye twiti hii:

Hongera sana kwa Samkeliso Kimbinyi, miaka 15, mwanafunzi wa kwanza kupata sifa za kituo cha mafunzo cha Microsoft katika utengenezaji wa zana

Mjadala Kuhusu Upatikanaji wa Mtandao wa Intaneti Wazidi Kushika Kasi Nchini Cuba

$
0
0
Foto Sandra Abd'Allah-Alvarez Ramírez

Picha na Sandra Abd'Allah-Alvarez Ramírez

Bila shaka yoyote, suala la mawasiliano nchini Cuba ni miongoni mwa mada inayofuatiliwa kwa ukaribu kabisa wakati huu. Kutokuwepo kwa namna rahisi na ya haraka ya kupata mawasiliano limekuwa si jambo linalozungumzwa sana katika kisiwa hiki, lakini pia mijadala imeshika kasi popote pale waishipo watu wa Cuba, na hii ni kutokana na umuhimu wa njia hii ya mawasiliano baina ya ndugu na marafiki.

Makala mbalimbali kuhusiana na tatizo la mtandao wa intaneti nchini Cuba zinasambaa katika mitandao mbalimbali nchini humo. Zifuatazo ni makala tatu miongoni mwa makala nyingi zinazosambazwa.:

ETECSA yatoa ufafanuzi

Alhamisi iliyopita, tarehe 16 Juni, maafisa kutoka kampuni ya mawasiliano ya Cuba(Empresa de Telecomunicaciones de Cuba, ETECSA), kampuni pekee nchini humo, iliweza kushiriki katika Jukwaa la mtandaoni lililoandaliwa na jarida la Cubasi.cu.

Wakati wa uwasilishaji mada, ETECSA iliweka bayana kuwa:

El posicionamiento de nuestros servicios es frecuentemente comparado con la asequibilidad y facilidades que ofertan los operadores de telecomunicaciones de otros países, incluidos los de la región de Latinoamérica. En la medida que se desplieguen las inversiones necesarias, nuestra empresa podrá lograr índices cada vez más comparables en cuanto a calidad y desarrollo,  y ampliará la infraestructura de telecomunicaciones, posibilitando la disminución de los precios y asimilando un mayor ritmo de crecimiento y diversificación de los servicios. 

Hali ya huduma ya mawasiliano katika nchi yetu mara nyingi imekuwa ikilinganishwa na urahisi wa upatikanaji na utoaji wa huduma hizi kutoka kwa wamiliki wa njia za mawasiliano kutoka nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na maeneo ya Amerika ya Kusini. Wakati ambapo uwekezaji muhimu unapoanza kuonekana, kampuni yetu itafikia kiwango cha ushindani kwa kuzingatia ubora na ubunifu, na hivyo miundombinu ya mawasiliano itaongezeka, hali itakayopelekea kupungua kwa gharama na kuwezesha kukua kwa haraka njia za mawasilino na utoaji wa huduma nzuri.

katika mijadala ya mtandaoni maswali yalijikita zaidi kwenye huduma za kitaifa za simu za mikononi, gharama na na upatikanaji wa huduma ya intaneti, wakizungumzia hali ya kutokuwapo kwa uwezekano wa kupata huduma ya intaneti watu wakiwa majumbani mwao. Katika mtazamo huu, Yosiel, aliuliza;

¿Por qué no es posible aún poner Internet en los domicilios a cubanos residentes en Cuba a precios asequibles?, y no me refiero a la infraestructura del típico desastre del Módem a 56 Kb con la inversión que esto necesita que además sabemos no es de buena calidad, me refiero a por qué no poner en cada central telefónica un buen o 4 buenos equipos de red inalámbrica y así cualquiera accedería desde su casa con su Smartphone, PC, Laptop, etc. A la red de redes a velocidades parecidas en salas de navegación de ETECSA misma.

Kwa nini hadi sasa huduma ya intaneti haijawezekana kupatikana kwenye makazi ya watu wa Cuba kwa gharama nafuu? Na hapa sizungumzii modem, kifaa hafifu kilicho na uwezo wa KB 56 na aina ya uwekezaji unaopaswa kuzingatiwa, ikizingatiwa pia na uzoefu tulionao, huduma hii haipo katika kiwango kinachotakiwa. Ninachokimaanisha hapa ni kuwa, ni kwa nini wasiweke chanzo kimoja au vinne vya mtandao wa intaneti wa si-waya ili kila mmoja aweze kupata huduma ya intaneti akiwa nyumbani kwake kupitia simu yake, ngamizi ya kawaida, ngamizi mpakato n.k ikiwa na kasi ifananayo na ile inayopatikana katika vituo vya ETECSA.

ETECSA responded:

La estrategia de ETECSA prevé el acceso a estos servicios desde los hogares; pero la prioridad inicial de la empresa ha sido ampliar las salas de navegación colectivas, para garantizar el acceso a un mayor número de personas.
En estos momentos, no resulta posible la generalización inmediata del acceso a Internet, dadas las limitaciones técnicas. No obstante, ETECSA se encuentra ejecutando inversiones que posibiliten la implementación de estos servicios con las condiciones técnicas requeridas y a precios inferiores a los actuales.

Mkakati wa ETECSA ni kuwa, siku zijazo mtandao upatikane hadi majumbani, hata hivyo, mpango wa awali wa kampuni ni kuongeza matawi yake ili watu wengi zaidi waweze kupata huduma.
Katika kipindi hiki, na kwa kuzingatia vikwazo vya kiufundi, haiwezekani kwa haraka kuwezesha watu kupata huduma ya intaneti wakiwa majumbani mwao. Hata hivyo, , ETECSA inaangalia namna ya utoaji wa huduma utakaochochea utoaji wa huduma kwa kuzingatia uwezo wa kiufundi na kwa gharama za chini zaidi ikilinganishwa na hali ilivyo sasa.

Tovuti zilizozuiwa: Zipitie leo, na labda sio kesho

Mnamo Juni 19, raia kadhaa pamoja na vyombo vya habari vilithibitisha kuwa, tovuti zilizokuwa zimezuiwa, zilianza tena kutumiwa kisiwani humo, miongoni mwa tovuti hizo maarufu, moja wapo ikiwa ni Skype. 

Majukwaa mengine ya kidigitali kama vile jarida la 14ymedio.com linalosimamiwa na mwanablogu Yoani Sánchez, ambalo kabla ya kurudishwa tena rasmi, lilielekezwa yoanilandia.com, hali iliyopelekea kushindikana kwa jarida hili kutembelewa na watu wakiwa kisiwani humu (hali iliyopingwa vikali) limekuwa tena likipatikana kupitia mtandao wa intaneti nchini Cuba. Revolico.com, jukwaa la biashara ya kupitia elekroniki la Cuba linaloshabihiana na craigslist, pia lilianza kupatika mtandaoni kwa watembeleaji waishio Cuba. Hata hivyo, mnamo Juni, 20, baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook walipelekewa ujumbe kuwa, tovuti hizi zimeshazuiwa tena. Nchini Cuba, msemo maarufu unasema kuwa, “Furaha katika nyumba ya mlala hoi haidumu”  

Uhuru wa upatikanaji wa huduma ya intaneti

Kimantiki,gharama za upatikanaji wa mtandao wa intaneti kwa watu wa Cuba zinaelezewa na Mhandisi wa masuala ya mawasiliano, Norges Rodriguez, ambaye pia ni mmiliki wa blogu ya  Salir a la manigua, anatembeza hati ya makubaliano ya mtandaoni katika Change.org, yanayoilenga mamlaka ya Cuba, hususani Waziri wa Mawasiliano, Maimir Mesa Ramos.

Miongoni mwa sababu za ombi hili ni:

Por  la trascendencia de las nuevas prácticas sociales que ofrece Internet que puede ser comparada solo con las que ofrecieron en su momento la aparición de la escritura, la imprenta, la radio, la telefonía, la televisión, y negarla sería negar el desarrollo.

Mambo mapya yanayofanyika hivi sasa miongoni mwa wanajamii yaliyowezeshwa kwa uwepo wa mtandao wa intaneti ni mambo ya kuzingatia na yale tu yawezayo kulinganishwa na yale yaliyokuwa yanatolewa kwa wakati wao. Utendaji Mpya wa kijamii uliowezeshwa na mtandao wa intaneti ni msingi na unaweza kufananishwa na ule unaoletwa, kwa wakati wake, yaweza kuwa uharaka wa uandikaji, uandishi wa habari, redio, huduma za simu, kuzuia mambo haya ni sawa na kuzuia maendeleo.

Katika suala hili, jambo hili linaonekana kuwa ni geni pale ambapo mwanablogu kutoka katika kisiwa hiki kuanzisha kampeni za mtandaoni. Siku za nyuma, kampeni ya mtandaoni iliyokuwa na lengo kama hili ilipewa nafasi kubwa Nchini Cuba, tunahitaji gharama muafaka za upatikanaji wa mtandao wa intaneti katika simu za mkononi lakini ni kutoka Florida, Marekani, katika wavutiCubanet

Trinidad & Tobago: Je, Kuishi kwenye Enzi za Kidijitali Kunahatarisha Haki yako ya Faragha??

Dondoo 13 za Kulinda Taarifa zako Kwenye Kompyuta Zinazotumiwa na Watu Wengi

$
0
0
ordenadores-publicos-300x234

Picha kutoka blogu ya profesoradeinformatica.com, imetumiwa kwa ruhusa.

Kama uko mbioni kwenda kwenye mapumziko na unafikiri kuchukua kompyuta yako na kuiunganisha na mtandao wa intaneti wa Siwaya (Wi-Fi) au kutumia kompyuta ambazo zinapatikana kwenye hoteli au kwenye eneo lolote la umma, unahitaji kusoma makala hii yenye dondoo 13 za kulinda taarifa zako, kama ilivyochapishwa na Andrea kwenye blogu yake:

¿Conoces los riegos de utilizar ordenadores públicos?

Desconoces el “estado de salud” de estos ordenadores, es decir estos pueden tener virus o programas maliciosos instalados para robar tu información (malwares). Entonces si no quieres que el estrés post-vacacional sea más agudo por problemas con tu información, lee con atención.

Unajua hatari ya kutumia kompyuta za umma?

Unapuuza ‘hali ya usalama wa kiafya’ wa kompyuta, na zinaweza kuwa na virusi au hata programu maalumu za kuiba taarifa zako. Kwa hiyo kama kutaki kuja kuchanganyikiwa baada ya kumaliza likizo yako na unataka kuwa makini zaidi na taarifa zako, soma kwa makini.

Hakuna wasiwasi kuhusu suala hili, sasa, namba 13 itakuwa ndiyo namba ya bahati zaidi.

Makala hii ilikuwa sehemu yetu ya saba ya #LunesDeBlogsGV (Jumatatu ya Blogu kwenye GV) ya tarehe 16 Juni, 2014. 

Highway Africa 2014 Yasogeza Mbele Tarehe ya Mwisho ya Kujiandikisha

$
0
0

Tarehe ya mwisho ya kujiandikisha kwa ajili ya Mkutano wa 18 wa mwaka wa Highway Africaimesogezwa mbele mpaka Ijumaa, Agosti 08 2014:

Kutokana na kuongezeka kwa shauku ya watu kuhudhuria mkutano wa mwaka wa 18 wa Highway Africa, tarehe ya mwisho ya kujiandikisha imesogezwa mbele mpaka Ijumaa, 08 Agosti 2014.

Mkutano huo mkubwa wa mwaka wa Waandishi wa Kiafrika unafanyika kwenye Chuo Kikuu cha Rhodes, Grahamstown, Afrika Kusini, kuanzia Septemba 7 – 8 2014.

Mkutano huo ukiwa na kauli mbiu, “Mitandao ya Kijamii – kutoka pembezoni mpaka kwenye vyombo vikuu”, utakuwa ukichambua namna mitandao ya kijamii ilivyoathiri maeneo yote ya maisha yetu katka kipindi cha miaka 10 iliyopita.


Viewing all 55 articles
Browse latest View live