Quantcast
Channel: Global Voices in Swahili » Teknolojia
Viewing all 55 articles
Browse latest View live

Sera ya Taarifa ya Uwazi Yahitaji Kuboreshwa zaidi Nchini Japan

$
0
0
Open Data Index

Screenshot of Open Data Index

Pamoja na kuwa serikali ya Japan inajitahidi kupiga hatua katika uboreshaji wa sera yake ya uwazi, nchi hii bado ina safari ndefu, kwani imeshika nafasi ya 30 kati ya nchi 70, kwa mujibu wa orodha liyoandaliwa na Asasi ya Ujuzi Huru. Masahiko Shoji wa Asasi ya Ujuzi Huru nchini Japani aandika:

日本は、政府支出、企業登記情報、交通時刻表、立法の分野で低い評価を受けました。また、どの項目もオープンライセンスの採用については「Yes」の評価を得ませんでした。これらの課題は6月に発表されたG8諸国における速報の時点と同じであり、日本の取り組みが大きくが進んでいないことを表しています。

Taaarifa huru za Japani kuhusiana na matumizi ya serikali, usajili wa makampuni, ratiba za usafiri na vyombo vya mahakama vilipata uungwaji mkono usioridhisha. Sehemu za taarifa hizi hazikupata tathmini ya “ndio”. changamoto kama hizi zinafanana na zile za viwango vya wanachama wa kundi la G8 vilivyotolewa mwezi Juni mwaka huu na Asasi ya Ujuzi Huru inayoonesha kuwa juhudi za Japani za kuboresha sera ya uwazi bado ni ndogo.

Kujua zaidi kuhusu vigezo vinavyozingatiwa katika kuweka viwango, tafadhali tembelea here

MATOKEO: Tuzo za Kwanza za Uandishi wa Kiraia Kuwahi Kutolewa Uganga

$
0
0

Tuzo za kwanza za uandishi wa kiraia Uganda (SMAs) zilitolewa kwa mara ya kwanza Novemba 15, 2013 kwenye sehemu ijulikanayo kama The hub, kwenye maduka ya Oasis jijini Kampala, Uganda.

Social Media Awards 2013 banner.

Bango la Tuzo za Uandishi wa Kiraia za mwaka 2013.

Malengo ya tuzo hizo, ambayo iliandaliwa na BluFlamingo, yalikuwa:

Tuzo hizi za Uandishi wa habari za kiraia za tukio la kwanza linalotafuta kuwaleta pamoja watu binafsi na mashirika ambayo yako mstari wa mbele linapokuja suala la kutumia vyombo vya habari za kiraia kwa minajili ya burudani, kuleta mabadiliko, kubadilishana mawazo, kutengeneza jumuiya na kuwasiliana na wateja mtandaoni.

Tuzo hizo zinatafuta kuwatuza watu na mashirika yanayofanya jitihda za dhati kuupa nguvu uandishi wa kiraia ili kuhusika na kujenga jumuiya mtandaoni. Kutokea kwenye watumiaji wa Facebook mpaka watumiaji wa mtandao wa twita na wanablogu wanaojituma.

Tukio hili la kwanza la aiana yake litafanyika Novemba 15 2013 na litawaleta si tu watu wanaojua masuala ya kidijitali, lakini pia mashirika makubwa yaliyo mstari wa mbele katika uandishi huu mpya na wale walishiriki katka kukuza uandishi wa habari za kiraia nchini Uganda.

Washindi wa kila kundi walikuwa kama ifuatavyo:

Tovuti bora ya burudani – BigEye
Mwandishi bora wa Burudani – Moses Serugo
Mwanablogu bora – Beewol

Kampuni kubwa bora – MTN Uganda

News & kampuni ya habari – NTV Uganda
News & habari za watu – Songa Stone

Huduma za Umma bora – Mamlaka ya Jiji la Kampala
Ubunifu bora – Matatu
Huduma bora za wateja – Airtel Uganda

Haki za jamii – Wanasheria pekupeku Uganda
Tuzo ya Udhibiti ya Majanga – Shirika la Taifa la MajiSafi na MajiTaka
Shirika bora la kuchapisha habari – The Red Pepper

Radio bora – Power FM
Runinga bora – NTV Uganda
Mtu maarufu – Anne Kansiime

Upigaji picha – Echwalu Photography
Kampeni bora ya uandishi wa kiraia – 40 & tabasamu 40
Chaguzo la Jaji – Proggie Uganda

Washindi walipendekezwa kupitia upigaji kura wa mtandaoni na baadae walichaguliwa na jopo la Majaji watano.

Wa-China Wametafuta Nini Zaidi Mtandaoni mwaka 2013

$
0
0

Mtandao wa kutafutia habari mtandaoni nchini China uitwao Baidu umetoa orodha ya maneno yaliyotumika zaidi kusaka habari. Orodha ya maneno kumi yaliyotumika zaidi ni kama ifuatavyo:

  1. Hali ya Hewa
  2. Taobao (tovuti ya kufanyia manunuzi ya mtandaoni nchini China)
  3. Wu Dong Qian Kun (kitabu cha mtandaoni cha Li Hu)
  4. The Tang Door  (kitabu cha mtandaoni)
  5. Mang Huang Ji (kitabu cha mtandaoni)
  6. Zhe Tian (kitabu cha mtandaoni)
  7. Double Chromosphere (Mchezo wa kamari wa Kichina)
  8. Baidu (!)
  9. Da Zhu Zai (kitabu cha mtandaoni)
  10. Qzone (a new mtandao wa kijamii from Tencent)

Kwa orodha kamili, fuatilia mtandao wa  China Internet Watch.

 

Uvumbuzi: Kompyuta Inayotumia Nishati ya Jua Nchini Mali

$
0
0
Limmorgal, a low power PC made in Mali via Tech of Africa with permission

Limmorgal, Kompyuta inayoendeshwa kwa nishati ya jua iliyotengezwa nchini Mali na Kampuni ya Tech of Africa kwa ruhusa

Kama sehemu ya mfululizo wetu juu ya teknolojia na ugunduzi unaofanyika Afrika, hivi karibuni tulionyesha Mashine ya Kuchapishia picha zenye umbo halisi yaani 3D iliyotengenezwa kutokana na taka pepe nchini Togo na mashine ya kukagua usahihi wa maneno katika lugha ya spell ki-Bambara . Leo, tunawaletea kompyuta ya kwanza kutumia umeme mdogo iliyotengenezwa nchini Mali. Kompyuta hiyo inayoitwa Limmorgal (ikiwa na maana ya kikokotozi kwa lugha ya ki-Peul) ni zao la bongo za vikundi viwili vya raia wa Mali, Jumuiya ya Intaneti Mali (ISOC Mali) na Intelec 3. Mamadou Iam Diallo, rais wa ISOC Mali, anaeleza mahitaji wanayohitaji kuyatatua kwa kutumia kompyuta hiyo akiongea na Blogu ya Bamako[fr]:

Nous avons conçu cette machine pour contribuer à la réduction du fossé numérique, mais également à la vulgarisation de l’outil informatique surtout en milieu scolaire. Limmorgal est aussi un ordinateur adapté à l’alimentation par l’énergie solaire grâce à sa faible consommation d’énergie.

Tulibuni kompyuta hii kusaidia kupunguza pengo kati ya walio mtandaoni na wale wasiomudu huduma za kidijitali, lakini pia  upanuzi wa matumizi ya kompyuta mashuleni. Limmorgal ni kompyuta ilitengenezwa mahususi kutumia umeme wa nishati ya jua na inatumia nishati kidogo sana (Watt 24 tu zinahitajika).

Sifa za kompyuta hiyo ni kama ifuatavyo :

  • Mfumo wa Ufanyaji kazi (Operating system): Ubuntu (zana huru) 
  • Uwezo wa kutafuta ni 1.4 G Hertz
  • 1GB RAM
  • Bei : 171000 Fcfa (Tsh 650,000 hivi)

Rais wa Korea Kusini Aapa Kupambana Uzushi Unaoenezwa katika Mitandao ya Kijamii

$
0
0

Je, serikali ya Korea Kusini imejiandaa kwa kufuatilia mitandao ya kijamii? Matamshi ya hivi karibuni ya Rais Park (full transcript [ko]) yamewashitua wa-Korea wanaotumia mtandao. Park, akiwalenga “uvumi ule unaosambaa kupitia mitandao ya kijamii”, alisema “kama serikali ikiachia mambo haya yakaendelea, itakuwa ghasia nchi nzima” na kuongeza “kumbukeni mamlaka za nchi zinahitaji kuchukua hatua kwa haraka sana na  kwa hisia zinazotakikana dhidi makundi yale yanayoharibu hali ya hewa”. Watumiaji wengi wa mtandao wa twita walipigia kelele wasiwasi wao na kuonyesha ukweli (kama twiti ya @ppsskr [ko] ambayo ilizunguka zaidi ya mara 500) kwamba vyombo vya serikali vimelituma zaidi ya twiti milioni 24 ili kumpa nafuu Park   wakati wa uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni.

Mwaliko wa Mapendekezo ya Tuzo za Blogu Nchini Kenya 2014

$
0
0

Waandaaji wa Tuzo za Blogu nchini Kenya 2014, ambao ni Umoja wa Wanablogu nchini humo (BAKE) kwa sasa wanakaribisha mapendekezo ya wawaniaji wa tuzo hizo mpaka Februari 10, 2014.  Watumiaji wanaweza kupiga kura kwa njia ya mtandao kuanzia Machi 1, mpaka April 30, 2014 kupendekeza blogu wanazoona kuwa ni bora katika makundi 17 tofauti, ikiwa ni pamoja na kundi jipya la Blogu bora ya Afya na Blogu Bora ya Kaunti/Wilaya.

Bake logo

Nembo rasmi ya BAKE. Picha imetolewa: http://bloggers.or.ke.

Tuzo za Blogu nchini Kenya,  ni mradi wa  Umoja wa Wanablogu wa Kenya (BAKE) , wanakusudia kuwazawadia wnaablogu wanaobandika posti zao mara kwa mara, wenye maudhui sahihi na yenye kusaidia, wabunifu na wenye mambo mapya. Makundi mengine ni pamoja na: 

  • Blogu bora ya Teknojia
  • Blogu bora ya Picha
  • Blogu bora ya Uandishi wa Kiubunifu
  • Blogu bora ya Biashara
  • Blogu bora ya Chakula
  • Blogu bora ya Kilimo/Mazingira
  • Blogu bora ya Mitindo/Urembo/Nywele
  • Blogu bora ya Siasa
  • Blogu bora Mpya
  • Blogu bora ya Shirika
  • Blogu bora ya Mada
  • Blogu bora ya Michezo
  • Blogu bora ya Burudani/Mtindo wa Maisha
  • Blogu bora ya Kusafiri/li>
  • Blogu bora ya Mwaka nchini Kenya

Hapa chini kuna video ya kuzinduliwa kwa Tuzo za Blogu Nchini Kenya:

Blogu zinaweza kupendekezwa kwa kutumia kiungo hiki.  

Shindano la Kuchochea Uanzishwaji wa Biashara Mpaya Nchini Madagaska

$
0
0

Harinjaka, mwanzilishi wa mradi wa Habaka na mwanablogu anayeishi Madagaska, ameanzisha Shindano la biashara mpya Antananarivo 2014  [fr] lenye lengo la kuchagua na kuunga mkono wazo la biashara nchini Madagaska. Anaamini kwmaba kuna  mustakabali mzuri kwa ujasiriamali na ubunifu [fr] nchini Madagaskari. Hapa unaweza kuona tangazo la tukio hilo[fr] :   

"The objective of the Start Up Cup is to connect founders with business investors and VCs." on the Facebook Page of the event

“Lengo la Shindano hilo la miradi mipya ni kuwaunganisha waanzilishi wa biashara hizo na wawekezaji na wadau wengine” kupitia Ukurasa wa Facebook wa tukio hilo kwa ruhusa

Wiki ya Mitandao ya Kiraia Jijini Lagos 2014

$
0
0

Wiki ya Mitandao ya Kiraia jijini Lagos 2014 (Februari 17-21) inaendelea jijini Lagos, Niajeria:

Wiki ya Mitandao ya Kiraia Lagos ndio kwanza mwaka wake pili kufanyika na tayari imepata umaarufu kama mkutano mkubwa zaidi wa kiteknolojia, mitandao ya kijamii na kibiashara barani Afrika. Tukio hilo limevutia wanazuoni maarufu, bidhaa maarufu, watu wajifunzao na wabunifu maarufu. Likiwa na idadi ya watu wapatao milioni 20, Lagos ndilo jiji kubwa la watu weusi duniani na inasemekana ni kitovu cha bara la Afrika na makazi ya makampuni makubwa ya kibiashara na kiteknolojia katika bara la Afrika. Kw akutambua umuhimu wa bara hili kuunganishwa, na kuhamasisha ushirikiano, dhima kuu ya mkutano wetu wa mwaka 2014 ni: AFRIKA ILIYOUNGANISHWA NDIYO MUSTAKABALI.

Tukio la pekee na la aina yake, Wiki ya Mitandao ya Kiraia Lagos ni mkutano wa kidunia unaohudhuriwa na watu wenye bongo zinazochemka kwa kiwango cha kidunia ambao hauna kiingilio na uko wazi kwa yeyote. WMK Lagos ni wa pekee kwa sababu asilimia 70 ya majopo, dhifa na warsha zimeandaliwa na umma


Tafakuri kwenye Mkutano Mkubwa Zaidi wa Blogu Nchini India

Vyombo Vikuu vya Habari Vyaihujumu Facebook

$
0
0

Mwanablogu wa Teknolojia Amitha Amarasinghe anadai kwamba mtandao wa Facebook unapewa taswira hasi na vyombo vikuu vya habari nchini Sri Lanka kwa vichwa vya habari kama “Mwanafunzi ajiua shauri ya picha iliyowekwa Facebook”, “Mapenzi ya Facebook yaishia na kifo” na kadhalika.

Ghafla tu, kuna mwongezeko mkubwa wa maudhui yanayotoa taswira hasi ya mtandao wa Facebook na Mitandao mingine ya kijamii. Kama ukichunguza habari hizi, [utagundua kuwa] vyombo vya habari vya hapa vinaitumia “Facebook” kama sehemu ya “habari”, lakini vikishindwa kuoanisha sababu za kijamii, kitamaduni, na kisiasa zinazosababisha matukio hayo.

Picha Mpya ya Korea Kaskazini ya Shirika la Anga la Marekani

$
0
0

Wasomaji wa kimataifa wanaofuatilia masuala ya Korea Kaskazini labda wangekutana angalau mara moja na picha hii maarufu ya rasi ya Korea kutoka Shirika la Anga la Marekani (NASA) kuonesha tofauti kubwa ya taa zinazoangaza usiku kwenye nchi hizo mbili za Korea. NASA hatimaye walihuisha picha zao za Satelaiti na ‘ina mwonekano mzuri kuliko picha ya zamani ya NASA', inaandika blogu ya Teknolojia ya Korea Kusini. Blogu hiyo pia inatambulisha toleo la video la picha hiyo linaloonyesha  Korea Kaskazini katika mukhtadha wa eneo lote la Asia Kaskazini. 

Global Voices Yaanzisha Ushirikiano na Shirika la Kukutanisha Wakimbizi

$
0
0

Refugees United

Wakimbizi Wakutanishwa

Hivi sasa dunia imeunganishwa zaidi kuliko ilivyowahi kuwa kabla, lakini wakati maelfu ya wakimbizi wanazikimbia nchi zao zenye migogoro au majanga na hivyo kupoteza mawasiliano na ndugu na jamaa zao -ambao mara nyingi hupoteza mawasiliano hayo milele. Katika wakimbizi 43 duniani kote, wengi wao wanasemekana hawaweza tena kuonana na familia zao tena kwa sababu tu ya kukosa namna ya kuwasiliana nao.

Refugees United[Wakimbizi Wakutanishwa] ni shirika ambalo hutumia mtandao wa intaneti na simu za kiganjani kusaidia familia zilizopoteana. Watumiaji wa mfumo wao huweka taarifa zao binafsi wanazoona ni salama kuzitangaza hadharani ambazo bado ziwafanye wabaki kuwa na faragha ya kutokufahamika. Watu wengi tayari wameshakutana na familia na marafiki zao kupitia mfumo huu wa Shirika la Wakimbizi Wakutana, lakini kuendelea kwa mafanikio hayo kutategemea ni jinsi gani wakimbizi watajua kuwa kuna kitu kama hicho.

Watafikiwaje?

Tangu mwaka uliopita, watafsiri wa Global Voices wamekuwa wakifanya kazi na shirika hilo la kukutanisha wakimbizi kwa kutafsiri vitendea kazi vyao, kutumia mitandao ya kijamii na ujumbe mfupi wa meneno (SMS) kwenda katika lugha za Kiswahili, Kifaransa, Kisomali, Kiamhari, Kiarabu cha Sudani na Kiarabu asilia. Tumeshirikiana nao kuwapa ushauri mahsusi kwa maeneo yanayolengwa kuhusu namna ya kutunga ujumbe unaoeleweka na unaokubalika kiutamaduni.

Shirika la Refugees United linasema linalenga kufikia watu milioni 1 ifikapo mwaka 2015 na Global Voices inajisikia fahari kutoa ushirikiano wa karibu.

“Ushirikiano na Global Voices ni ushahidi wa namna tunavyoweza kuzifikia familia nyingi zaidi kwa kushirikiana na mtandao wao imara wa watafsiri na wanablogu,” anasema Ida Jeng wa shirika hilo la Refugees United.

Nguvu ya kuungana kwa mara nyingine

Kwenye blogu ya Refugees United kuna masimulizi yasiyohesabika kuhusu miradi ya kuwafikia watu na namna watu waliopoteana walifanikiwa kukutana kwa mara nyingine.

Video hii inaelezaea simulizi la mwanamke aitwaye Estelle aliyekutana na dada yake baada ya kutengana naye kwa miaka 16.

Na video hii inawaonyesha kaka wawili wa ki-Kongo waliotengana kwa miaka 15 na hatimaye kukutana kwa mara ya kwanza kwenye zana ya mtandaoni ya Google Hangout on Air baada ya kufahamishana mahali walipo kupitia mtandao wa shirika la Refugees United.

Mazungumzo ya GV: Heri ya Miaka 25 ya Kuzaliwa, Mtandao!

$
0
0

Ni mwaka wa 25 tangu kuzalwia kwa Mtandao wa Intaneti Unaopatikana Duniani kote ujulikanao kama “World Wide Web”! Katika toleo hili la Mazungumzo ya GV, wakongwe wa Global Voices wanazungumzia uzoefu wao wa zamani katika mtandao wa Intenati na yale yote yaliyowezeshwa na mtandao huo katika miaka (karibu) kumi ya shirika hili. Alan Emtage, mtengenezaji wa mtandao na mbunifu wa Archie, mtandao wa kwanza wa kutafutia maudhui kwenye intaneti, anazumngumza nasi kutoka Barbados kuhusiana na uzoefu wake kama mwanzilishi wa Mtandao. Na Kiongozi wa jumuiya wa GV Renata Avila na Mkurugenzi wa Kampeni ya Uandishi Huru wa Mtandaoni Josh Levy wanatuambia kuhusu kampeni ya Mtandao Tunaoutaka,  mradi mpya unaowezesha mazungumzo ya kidunia kuhusu haki za mwanadamu na Mtandao wa Intaneti.

Flipboard Yaiongeza Global Voices Kwenye Mwongozo wake wa Maudhui

$
0
0
Flipboard Italian content guide

Watumiaji wa Kiitalia wa mtandao wa Flipboard wataikuta Global Voices ikiwa kwenye orodha ya habari zinazopendekezwa.

Kuanzia mwezi huu, mtandao wa Global Voices (katika lugha tofauti) utakuwa ukipendekezwa kwa mamilioni ya watu wanaotumia zana tumizi iitwayo Flipboard kwenye simu zao za kisasa au vifaa vingine vya kielektroniki ili kutengeneza kitu kinachofanana na “gazeti” kitakachokusanya mitandao yenye mvuto na maudhui ya mitandao ya kiraia katika sehemu moja.

Kwa mfano, watumiaji wa Kiitalia watapendekezewa Global Voices Kiitalia, na watumiaji wa mtandao wa Flipboard watapendekezewa Global Voices Kireno . Unaweza kuona namna inavyoonekana unapoperuzi mtandao wa Global Voices katika mtindo wa gazeti hapa.

Mtandao wa Flipboard unasema Global Voices itaongezwa kwenye mwongozo wa maudhui kwa watumiaji wanaoishi Japan, Hong Kong, Taiwan, Ufaransa, Uhispania, Brazil, Italia, Urusi, Uarabuni.

Mtandao wa Global Voices kwa sasa unapatikana katika zaidi ya lugha 30 tofauti shukrani za pekee kwa wahariri na wafasiri wetu wanaojitolea kwenye mradi wetu wa Lingua. Kwa pamoja, tunafanya kazi ili kufikia lengo la kuzifanya habari zetu na mitandao yetu ya kiraia kutoka duniani kote kuifikia hadhira ya dunia nzima. Ungana nasi!

Teknolojia ya Kiafrika: Mradi wa TechAfrique Watathmini Hatua Iliyofikiwa

$
0
0

 Le continent africain apparaît comme la nouvelle frontière mondiale du développement numérique. Ce développement provoque une nouvelle impulsion entrepreneuriale en Afrique, et notamment en Afrique francophone. Mais ce potentiel reste très largement méconnu en Europe ainsi qu'en France. 

Bara la Afrika linaonekana kuwa kiongozi mpya wa dunia katika maendeleo ya kidijitali. Maendeleo haya yamesababisha kukua kwa ujasiria mali mpya barani Afrika, hususani kwenye nchi zizungumzao Kifaransa. Lakini uwezo huu unabaki kuwa siri isiyofahamika huko Ulaya na Ufaransa.

Kubadili hali hii, Samiri, mwandishi wa blogu ya  Startup BRICS [fr] ilijikita kwenye miradi mipya katika nchi zinazoendelea, aliandaa safari za kiuchunguzi zilizoitwa  Mradi wa TechAfrique ili kugundua na kuorodhesha miradi iliyopo na ile mipa, miradi ya Fablabs, na kwenye maeneo mengine yanayofanana na hayo katika ubunifu wa kiteknolojia katika nchi zizungumzao Kifaransa pamoja na Kenya.


Shule 2,715 Kuunganishwa na Mtandao wa Intaneti Nairobi

$
0
0

Shule 2,715 jijini Nairobi, Kenya hivi karibuni zitaunganishwa na mtandao wa intaneti wa bure:

Wanachi Group [kampuni] imefikia makubaliano ya kutekeleza mradi wa thamani ya Dola za Marekani milioni 3 (Takribani KSh milioni 270) na kaunti ya Nairobi, ili kuunganisha shule 2,715 jijini Nairobi na mtandao wa intaneti.

Mradi huo ulizinduliwa leo na ifikapo mwezi Juni mwaka huu (ndio, ndani ya miezi mitatu), shule 245 za mfano zinatarajiwa kuwa zimeunganishwa tayari. Baada ya hapo, mradi huo utatathiminiwa na awamu ya pili itaanza ndani ya miaka mitatu hadi mitano.

“Pamoja na mtandao wa bure wa intaneti, kampuni hiyo itaipatia kila shule vifaa vya kidijitali kwa ajili ya kuunganisha televisheni kwa ajili ya matumizi ya kupata maudhui ya elimu kwa njia ya sauti kwa faida ya wanafunzi. Watoto wa shule za awali watapata vifaa hivyo pia ikiwa ni pamoja na televisheni ndogo,” ilisema taarifa ya kampuni hiyo ya Wananchi.

Fasiri ya Lugha ya Kikannada ya Karne ya 11 Yapatikana kwenye Mfumo wa Wikisource

$
0
0

Vachana Sahitya ni aina ya uandishi kwa mtindo wa sauti katika lugha ya ki-Kannada ambao ulianzia karne ya 11 na kukua sana kwenye karne ya 12. Makala ya Subhashish Panigrahi inaripoti (ikiwa imeandikwa kwa ushirikiano wa Pavithra Hanchagaiah na Omshivaprakash) kwenye blogu ya Wikimedia kwamba waandishi wawili wa Wikimedia wakishirikiana na mtaalamu wa lugha ya ki-Kannada wamegeuza beti 21000 za Vachana Sahitya katika mfumo wa Unicode na hiyo kwa sasa zinapatikana kwneye Wikisource, maktaba ya kidigitali ya mtandaoni ambayo ina maudhui ya nyenzo za maandishi yanayopatikana bure.

Maombi ya Mtandao wa WeChat na ‘Self-Media’ kwa Raia wa China

$
0
0

Mitandao ya ’s , huduma ya ujumbe binafsi kwa namna fulani imechukua nafasi ya mtandao unaofanana kidogo na Twita uuitwao Sina Weibo kama chombo kinachoongoza kwa mawasiliano mbadala. Mtandao wa Tea Leaf Nation  umeelezea maombi ya mtandao wa WeChat na “self-media” kwa ujumla/a> kwa kizazi cha Wachina vijana, na maana ya  hatua yake ya dharura/a>. 

Twiti ya kwanza kutoka kwa Rais wa Madagaska

$
0
0
Madagascar president Hery Rajaonarimampianina - Public domain

Rais wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina – Picha ya matumizi ya umma

Rais mteule wa Madagaska Hery Rajaonarimampianina amefungua akaunti yake ya mtandao wa twita mnamo tarehe 23 Machi, 2014. Hii ndiyo twiti yake ya kwanza : 

First tweet by president of Madagascar

Twiti ya kwanza ya rais wa Madagaska

Kuna uwezekano mkubwa kuwa hiyo ndiyo twiti maarufu kutoka kwa mkuu wa nchi. Ni Rupert Murdoch anaweza kuwa na wasiwasi na kiwango cha “ukubwa/umaarufu” wa twiti yake ya kwanza. Rais wa Madagaska ana sifa yake ya pekee kuwa mkuu wa nchi mwenye jina refu kuliko wengine /a>.

Namna Huduma ya Kuhamisha Fedha kwa Njia ya Simu Ilivyobadili Maisha ya Wakenya

$
0
0
M-Pesa payment till at a restaurant in Kenya. Photo released under Creative Commons by Wikipedia user Raidarmax.

Mahali pa kufanyia malipo ya M-Pesa kwenye hoteli nchini Kenya. Oicha imetolewa chini ya leseni ya Creative Commons na mtumiaji wa Wikipedia Raidarmax.

Mwezi Machi 2014 yatakuwa ni maadhimisho ya miaka saba tangu M-Pesa, huduma ya kufanya miamala ya kifedha kwa njia ya simu na huduma ndogo za kibenki, ilipoanzishwa Kenya na kampuni ya simu za mkononi iitwayo Safaricom. M-Pesa inafanya kazi kama benki; watumiaji wa huduma hiyo huhifadhi fedha kwenye simu zao na kutoa fedha kupitia wakala au duka la Safaricom kwa kuonyesha kitambulisho na namba ya simu.

Safaricom ilikuwa kampuni ya kwanza nchini Kenya kutoa huduma ya miamala ya kibenki. Inabaki kuwa  kampuni iliyotawala biashara hiyo hata leo, wakati kukiwa na makapuni kama Airtel, Orange na Yu ambayo pia yanatoa huduma kama hiyo.  Katika kusherehekea miaka saba ya huduma hiyo, Safaricom iliwahamasisha wa-Kenya kwenye mtandao wa Twita kutumia alama habari ya #BeforeMPESA [Kabla ya MPESA] kueleza namna huduma hiyo ilivyobadili maisha.

Hapa unaweza kusoma maoni yaliyojitokeza mara nyingi:

1. M-Pesa imewapa Wakenya mbadala wa kutunza fedha zao kwa usalama:

Kabla ya Mpesa

Kabla ya Mpesa: Namna watu walivyokuwa wakitunza fedha zao kwa usalama

2. Kenyans can now pay for almost anything through M-Pesa, even church offerings [sadaka] and electricity bills:

Ninaweza kulipa sadaka kwa urahisi nikiwa sebuleni kwangu, bila kulazimika kwenye kanisani

Hivi ndivyo nilivyokuwa nilisafiri kwenda benki kulipa bili yangu ya umeme

Kufupisha masimulizi huduma hii imefanya maisha yangu kuwa rahisi tangu nijiunge na Mpesa

Ukitoka kuzunguka, ukaishiwa na mafuta….unatembea mwendo mfupi tu unalipa na Mpesa

Baada ya kupata chakula na rafiki yako wa kike na kisha unakumbuka uliacha pochi yako nyumbani

Malipo ya mahari ilikuwa kazi…baada ya Mpesa sasa ni rahisi

Baadhi ya watu walizimia kwenye mistari mirefu benki wakati wa kufungua shule kwa sababu ya kuchoka kusubiri

Namna nilivyokuwa nikisubiri kutumiwa hawala ya fedha kwa njia ya posta

Kabla ya Mpesa na baada ya miaka saba ya Mpesa

3. M-Pesa inaweza kupatikana kwa simu yoyote:

@kebiwot Miaka saba ya MPESA lakini simu zina miaka 20

Bado, si kila mmoja anaifurahia M-Pesa

Baadhi ya Wakenya walitumia maadhimisho hayo kuonyesha hasira zao kwa M-Pesa na kuwakosoa wale wanaoisifia huduma hiyo:

Na hadithi hizi za kusadikika za MPESA

Namna Safaricom wanavyokuita kuja kukumaliza….

Samuel Gikuru alikuwa na wasiwasi na nia ya Safaricom na hata akaituhumu kampuni hiyo kuiba wazo la Mkenya alibuni huduma hiyo:

Hivi ni mimi pekeyangu au na mwingine amegundua kuwa Safaricom inafanya kila inachoweza kwa makusudi mazima kuua Vipaji vya kiteknolojia vinavyoibukia Kenya? Kuna hadithi inasimulia namna Mkenya alivyoibiwa wazo lake lenye thamani ya dola bilioni moja ambalo leo ndio limekuwa M-Psa. Kijana huyo mwenye akili inasemekana aliwaendea wakubwa wa Safaricom na wakamkatalia kuwa wazo lake lisingetekelezeka na ajabu miezi kadhaa baadae wakazindua huduma hiyo. Hiyo ndiyo hadithi iliyo kwenye midomo ya Wakenya wote. Hata hivyo, kitabu kipya kinadai kuwa mwajiriwa mwandamizi wa Vodafone ndiye aliyebuni M-Pesa mwaka 2003. Wakenya ni kama hawafaidiki na ubunifu wa M-Pesa ambao ndio unaiweka Kenya kwenye ramani ya dunia kama kituo cha ubunifu.

….Ukiwa na MPESA, faragha yako hailindiw. Kwa kutumia hela kidogo mpaka hata shilingi 10, mtu yeyote anaweza kukutambu kama mmiliki wa lini ya simu, kama namba yako imesajiliwa kwa huduma hiyo, kirahisi tu. Kama vile haitoshi watekaji wanaweza kutumia husuma hii kudai fedha. Ili kuhakikisha kuwa hawakamatwi au kuingia mtegoni kirahisi, wanafungua akaunti kwa kutumia kitambulisho bandia ambacho kinaweza kutengenezwa kinyume cha sheria pale kwenye mtaa wa River road Nairobi. Safaricom haifanyi chochote kuhakiki usahihi wa namba za kitambulisho.

Viewing all 55 articles
Browse latest View live